tg

Tuesday, April 2, 2013

WATU 20 WAHOFIWA KUFA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI ARUSHA KATIKA MGODI WA MORRUM




Picture

Picture

Taarifa  kutoka mkoani Arusha  zilizoufikia mtandao huu  hivi punde  zinadai kuwa watu 20 wanahofiwa kupoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa ndani ya mgodi wa Morrum huko Moshono jijini Arusha. 

Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .

Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.

Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni  Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16 waliofukiwa.

Baadhi ya miili ya marehemu  imetambulika kwa majina kuwa ni  Alex Maliaki, Gerald Hamis, Sauli Rafael (Mbu), Barick Loselian, Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na Garald Masai.

Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya mvua.

0 comments:

Post a Comment