tg

Saturday, March 30, 2013

MBUNGE WA CHAMBANI Zanziber CUF AmeFARIKI DUNIA


 
Mbunge wa Jimbo la Chambani  Visiwani Zanzibar kupitia tiketi ya CUF Salim Hemed Khamis aliyeanguka jana alipohudhuria katika vikao vya kamati za bunge jijini Dar es salaam na kupelekwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa zilizofikia mtandao huu zimeeleza kuwa mbunge huyo amefariki dunia.


Mbunge wa Chambani Kupitia Chama cha Wananchi CUF Ambaye Pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Salim Hemed Hamis Amefariki Dunia Hii Leo Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Alipokuwa Amelazwa Katika Chumba cha Uangalizi Maalum.

Hapo Jana Marehemu Salim Hemed Alianguka Ghafla Katika Ofisi Ndogo za Mbunge Jijini Dar Es Salaam na Kupelekea Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Mambo ya Nje Kusimamisha Kikao Chake Kwa Dharura.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Taifa CUF Prof. Ibrahim Lipumba Amethibitisha Kutokea Kwa Kifo Hicho Mchana wa Leo Alipoongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam.

Kwa Mujibu wa Taarifa Iliyotolewa na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila Amesema Maandalizi ya Kuusafirisha Mwili wa Marehemu Kwenda Pemba Kwa Ajili ya Maziko Yanafanyika.

0 comments:

Post a Comment