tg

Saturday, March 30, 2013

MADEREVA NA MAKONDACTA WAZIBA BARABARA BAADA YA LORI KUPAKI KATIKATI NJOMBE.


 
 Barabara ya Njombe Makete iliyozibwa baada ya lori kukwamisha safari ya magari mengine lililopakiwa tangu jana Jioni katika barabara hiyo eneo la Ruhuji Ramadhani Njombe.


 Hilo ndilo lori lililo paki barabarani baada ya kukwama na kisha kusababisha Foleni Kubwa katika eneo la Mlima wa kupandisha Ramadhani Njombe jirani kabisa na Mto Ruhuji.

 Vyombo vya ulinzi na Usalama Barabarani vikiwasili eneo la tukio ilikozibwa barabara na baadhi ya madereva waliokwamishwa safari zao na lori hilo tangu jana jioni.
 Afisa usalama barabarani[RTO]Mkoa wa Njombe Maro Chacha anayeonekana hapo akiwa eneo la tukio hilo ilikozibwa Barabara,




 Ukarabati wa Barabara hiyo ukiendelea lakini bado magari yameendelea kunasa kwenye tope na kisha kuendelea kuharibu barababara hiyo Njombe.
 Hali ya ulinzi na usalama ikiimarishwa katika eneo la Barabara ya Njombe Makete eneo la mlima Ruhuji kuelekea Ramadhani huku hata gari la Polisi nalo likinasa kwenye tope.
Pamoja na hali mbaya ya barabara hiyo inayoendelea kurekebishwa lakini magari yameendelea kupita yakiwa yamebeba mizigo na taka.
 
Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Mkoani Njombe Umesema Utaweka Mizani Katika Barabara ya Njombe Hadi Makete Ili Kuyadhibiti Magari Yenye Uzito wa Zaidi ya Tani Kumi Ambayo Yamekuwa Yakitumia Barabara Hiyo na Kusababisha Uharibifu wa Mara Kwa Mara.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Mhandisi Yussuph Mazana Amesema Wataalamu na Maafisa wa TANROADS Watakuwa Wakitembea na Mizani Hiyo Katika Barabara na Kupima Magari Yote Kabl ya Kuyabaini Yale Yote Yatakayokuwa Yamezidi Uzito na Kuchukua Hatua Zinazostahiki.

Hatua Hiyo ya TANROADS Inafuatia Malalamiko ya Mara Kwa Mara ya Wananchi Mkoani Njombe Hasa Watumiaji wa Barabara ya Njombe Hadi Makete Barabara Ambayo Imekuwa Ikiharibika Kutoka na Kutumiwa na Magarai Yaliozidi Uzito.

Katika Kile Kinachoonekana Kuwa ni Muendelezo wa Kero Zinazowakabili Wananchi Wanaotumia Barabara Hiyo,Hii Leo Zaidi ya Magari Mia Moja Yalikwama Kutokana na Hali Mbaya ya Barabara Katika Kipindi Hiki Ambacho Ukarabati Umekuwa Ukiendelea.

Baadhi ya Wananchi Pia Walilazimika Kuifunga Barabara Hiyo Kwa Saa Kabla ya Jeshi la Polisi Kufika Eneo Hilo na Kuruhusu Shughuli Nyingine.

0 comments:

Post a Comment