tg

Saturday, March 30, 2013

KESI YA KUMJERUHI DIWANI WA KATA YA RAMADHANI NJOMBE IMEENDELEA KUSIKILIZWA LEO.



 
 
Kesi ya Kumshambulia na Kumjeruhi Diwani wa Kata ya Ramadhan  Wilayani Njombe Alfred LuvandaInayomkabili Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Ramadhan Bw Erasto Ngole  Imesikilizwa Tena Leo Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe Kwa  Shahidi wa Tano wa Upande wa Mlalamikaji Kutoa Ushahidi Katika Mahakama Hiyo.

Akitoa Ushahidi Mahakamani Hapo , Shahidi Namba Tano Jimy Ngulwa Ambaye ni Kinyozi wa Ocean Saluni Ambako Lilitokea Tukio  Hilo Ameiambia Mahakama Kuwa, Wakati Mlalamikaji Akisoma Gazeti Akiwa Anasubiri Kunyolewa , Mshtakiwa Erasto Ngole Aliingia na Kuanza Kurushiana  Maneno na Mlalamikaji  Alfred Luvanda.

Shahidi Huyo Ameieleza Mahakama Kuwa Wakati Wakiendelea Kurushiana Maneno Baadaye Walishikana na Kisha Kuvutana Kuelekea Nje ya Saluni Huku Mshtakiwa Akitoka na Kiti Kidogo Aina ya Sturi Aliodaiwa Kuitumia Kumpiga Mlalamikaji.

Licha ya Upande wa Mlalamikaji Kuleta Sturi  Kama Kielelezo Kilichotumika Siku ya Tukio , Mshtakiwa Amekana Kuitambua Kama Kielelezo Hivyo Mahakama Kumruhusu Mlalamikaji Kuleta Kielelezo Kingine Ambacho ni CD Inayodaiwa Kurekodi Tukio Hilo.

Baada ya Ushahidi Huo Kutolewa Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Aprili 25 Mwaka Huu Itakaposikilizwa Tena Mahakamani Hapo na Mshtakiwa Yuko Nje Kwa Dhamana.

0 comments:

Post a Comment