Wafuasi hao wa Shekh Ponda wakipandishwa kwenye gari la polisi mara baada ya kukamatwa katika maandamano hayo.
Licha ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuzuia maandamano ya Waumini wa Dini ya Kiislam, baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni Waumini wa Dini hiyo katika maeneo ya Buguruni, Malapa na Kariakoo wamefanya maandamano hayo.
Hata
hivyo Jeshi la Polisi kupitia Vikosi vya Kutulia Ghasia-FFU-limelazimika
kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wamebeba Mabango
na Mawe kwenye Mifuko katika Mitaa ya Malapa pamoja na Kariakoo.
mtandao huu wa www.jamiiyanjombe.blogspot.com umeshuhudia Maduka mbalimbali yakiwa yamefungwa katika Mitaa
ya Kariakoo kutokana na maandamano hayo ya watu wanaodaiwa kuwa Waumini wa Dini
ya Kiislam.
Waumini
hao wanashinikiza Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka-DPP-kumwachia kwa
dhamana Katibu wa Jumuiya ya Waislam Shekh PONDA ISA PONDA ambaye anakabiliwa
na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Jana
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar e s salaam kupitia kwa Kaimu Kamanda wake
AHMED MSANGI lilipiga marufuku kufanyika kwa mandamano hayo kutokana na
kutokuwa na kibali cha Polisi.
0 comments:
Post a Comment