Barabara ya Njombe Makete
iliyozibwa baada ya lori kukwamisha safari ya magari mengine
lililopakiwa tangu jana Jioni katika barabara hiyo eneo la Ruhuji
Ramadhani Njombe.
Hilo ndilo
lori lililo paki barabarani baada ya kukwama na kisha kusababisha Foleni
Kubwa katika eneo la Mlima wa kupandisha Ramadhani Njombe jirani kabisa
na Mto Ruhuji.
Vyombo vya
ulinzi na Usalama Barabarani vikiwasili eneo la tukio ilikozibwa
barabara na baadhi ya madereva waliokwamishwa safari zao na lori hilo
tangu jana jioni.
Afisa usalama barabarani[RTO]Mkoa wa Njombe Maro Chacha anayeonekana hapo akiwa eneo la tukio hilo ilikozibwa Barabara,
Ukarabati wa Barabara hiyo
ukiendelea lakini bado magari yameendelea kunasa kwenye tope na kisha
kuendelea kuharibu barababara hiyo Njombe.
Hali ya
ulinzi na usalama ikiimarishwa katika eneo la Barabara ya Njombe Makete
eneo la mlima Ruhuji kuelekea Ramadhani huku hata gari la Polisi nalo
likinasa kwenye tope.
Pamoja na hali mbaya ya barabara hiyo inayoendelea kurekebishwa lakini magari yameendelea kupita yakiwa yamebeba mizigo na taka.
Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Mkoani Njombe Umesema Utaweka
Mizani Katika Barabara ya Njombe Hadi Makete Ili Kuyadhibiti Magari
Yenye Uzito wa Zaidi ya Tani Kumi Ambayo Yamekuwa Yakitumia Barabara
Hiyo na Kusababisha Uharibifu wa Mara Kwa Mara.
Meneja wa
TANROADS Mkoa wa Njombe Mhandisi Yussuph Mazana Amesema Wataalamu na
Maafisa wa TANROADS Watakuwa Wakitembea na Mizani Hiyo Katika Barabara
na Kupima Magari Yote Kabl ya Kuyabaini Yale Yote Yatakayokuwa Yamezidi
Uzito na Kuchukua Hatua Zinazostahiki.
Hatua Hiyo ya TANROADS
Inafuatia Malalamiko ya Mara Kwa Mara ya Wananchi Mkoani Njombe Hasa
Watumiaji wa Barabara ya Njombe Hadi Makete Barabara Ambayo Imekuwa
Ikiharibika Kutoka na Kutumiwa na Magarai Yaliozidi Uzito.
Katika
Kile Kinachoonekana Kuwa ni Muendelezo wa Kero Zinazowakabili Wananchi
Wanaotumia Barabara Hiyo,Hii Leo Zaidi ya Magari Mia Moja Yalikwama
Kutokana na Hali Mbaya ya Barabara Katika Kipindi Hiki Ambacho Ukarabati
Umekuwa Ukiendelea.
Baadhi ya Wananchi Pia Walilazimika Kuifunga
Barabara Hiyo Kwa Saa Kabla ya Jeshi la Polisi Kufika Eneo Hilo na
Kuruhusu Shughuli Nyingine.
0 comments:
Post a Comment