Kesi ya Kumshambulia na Kumjeruhi Diwani
wa Kata ya Ramadhan Wilayani Njombe Alfred LuvandaInayomkabili Katibu
Mwenezi wa CCM Kata ya Ramadhan Bw Erasto Ngole Imesikilizwa Tena Leo
Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe Kwa Shahidi wa Tano wa Upande wa
Mlalamikaji Kutoa Ushahidi Katika Mahakama Hiyo.
Akitoa Ushahidi Mahakamani Hapo , Shahidi Namba Tano Jimy Ngulwa Ambaye ni Kinyozi wa Ocean Saluni Ambako Lilitokea Tukio Hilo Ameiambia Mahakama Kuwa, Wakati Mlalamikaji Akisoma Gazeti Akiwa Anasubiri Kunyolewa , Mshtakiwa Erasto Ngole Aliingia na Kuanza Kurushiana Maneno na Mlalamikaji Alfred Luvanda.
Shahidi Huyo Ameieleza Mahakama Kuwa Wakati Wakiendelea Kurushiana Maneno Baadaye Walishikana na Kisha Kuvutana Kuelekea Nje ya Saluni Huku Mshtakiwa Akitoka na Kiti Kidogo Aina ya Sturi Aliodaiwa Kuitumia Kumpiga Mlalamikaji.
Licha ya Upande wa Mlalamikaji Kuleta Sturi Kama Kielelezo Kilichotumika Siku ya Tukio , Mshtakiwa Amekana Kuitambua Kama Kielelezo Hivyo Mahakama Kumruhusu Mlalamikaji Kuleta Kielelezo Kingine Ambacho ni CD Inayodaiwa Kurekodi Tukio Hilo.
Baada ya Ushahidi Huo Kutolewa Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Aprili 25 Mwaka Huu Itakaposikilizwa Tena Mahakamani Hapo na Mshtakiwa Yuko Nje Kwa Dhamana.

0 comments:
Post a Comment