Mwanzoni Mwa Mwaka Huu Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini TMA Ilitoa Taarifa Juu ya Uwepo wa Mvua za Juu Kwa Wastani Katika Baadhi ya Mikoa Ukiwemo Mkoa wa Njombe,Mvua Ambazo Pia Zilitabiriwa Kuwa Huenda Zingeweza Kuwa na Madhara Kwa Wananchi.
Katika Taarifa Yake ya Tahadhari Kwa Wananchi TMA Iliwataka Wananchi Hasa Wale Wanaoishi Maeneo ya Mabondeni Kuchukua Tahadhari Ikiwezekana Kuhama Kwenye Maeneo Hayo Kwani Kiwango Hicho Cha Mvua Kinaweza Kusababisha Madhara Kwao
Ingawa Mvua Zinazonyesha Kwa Sasa Mkoani Njombe Si Sehemu ya Mvua Zilizotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Lakini Bado Zimekuwa na Madhara Kwa Wananchi na Kwa Sehemu Kubwa Wanaokumbwa na Madhara Hayo ni Wale Walioendelea Kuishi Katika Maeneo ya Mabondeni.
Mitaa ya Mpechi na Kilimani Mjini Njombe ni Miongoni Mwa Mitaa Ambayo Tayari Imeanza Kukumbwa na Janga Hilo Ambalo Limesababisha Nyumba Zaidi ya Tisa Kuezuliwa Kutokana na Mvua Zilizonyesha Wiki Hii
Aidha Mvua Hizo Pia Zimesababisha Baadhi ya Wananchi Kuwa Katika Mazingira Magumu Baada ya Nyumba Zao Kupata Madhara Tofauti Ikiwemo Kuta Zake Kudondoka na Nyingine Kuezuliwa paa.
Baadhi ya Wananchi Waliozungummza na matukio Wanaonesha Wasiwasi Wao wa Kuendelea Kujitokeza Kwa Madhara Hayo Kwa Kuwa Sehemu Kubwa ya Wakazi wa Mitaa Hiyo Wamejenga Karibu Kabisa na Chanzo Cha Maji.
Wanaishauri Serikali Kuongeza Usimamizi Katika Sheria za Usimamizi wa Vyanzo Vya Maji Ambazo Wanadhani Zimekosa Usimamizi wa Kutosha Kwa Kuwa Ongezeko la Wananchi Wanaojenga Karibu na Vyanzo Vya Maji Limekuwa Likiongezeka Kila Siku
Kwa upande wao wadau wa maendeleo akiwemo balozi wa mtaa wa Mpechi kilimani Bwana Chiefu Mkongwa walikuwa na maoni tofauti dhidi ya mafuriko hayo.
Isabela Malangalila ni Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mpechi Anasema wananchi na wamiliki wa viwanja vinavyotarajiwa kujengwa kando ya mito hiyo wanatakiwa kuacha huku wale Wote walioko katika maeneo hatarishi ya kwenye vyanzo vya maji wakitakiwa kutafuta maeneo mengine ya kujenga ili wahame sehemu walizozijenga kuepukana na mafuriko hayo.
0 comments:
Post a Comment