tg

Sunday, July 28, 2013

ZAHANATI YA KIJIJI CHA IKONDO WILAYANI NJOMBE IMEFUNGWA KUTOKANA NA WAUGUZI KWENDA KWENYE SEMINA ....

0 comments






 TAARIFA YA KATA YA IKONDO ILIYOSOMWA NA AFISA MTENDAJI WA KATA HIYO







Zahanati ya Kijiji cha Ikondo katika kata ya Ikonda wilayani Njombe ilisimama kufanya kazi kwa muda wa siku ya mbili baada ya wauguzi na wakunga wa zahanati hiyo kufunga na kwenda kwenye semina mjini Njombe ambapo pamoja na mambo mengine wagonjwa wa kijiji hichowalikuwa hatarini kupoteza maisha kwa kukosa huduma za matibabu.

Wakizungumza Mbele ya Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini Bwana Deo Sanga wananchi wa kijiji cha Ikondo walilalamikia kufungwa kwa zahanati hiyo kutokana na kile kilicho daiwa kuwa madaktari walikwenda kwenye semina ya tarehe  23 na 24  huku wagonjwa wakiachwa pasipo kupatiwa huduma za matibabu.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa katika zahanati hiyo wanakabiliwa na changamoto mbali,mbali ikiwemo ya ukosefu wa nyumba za waganga,ukosefu wa dawa zikiwemo za kuvubaza makali ya virusi vya UKIMWI na kwamba kwa sasa wanasafiri umbali wa zaidi ya kilomita 50 kwenda kupata tiba hiyo kutokana na zahanati hiyo kuwa haina uwezo wa kutoa huduma hiyo.
 
Akizungumzia tatizo la kufungwa kwa zahanati hiyo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Filbert Mbwiro amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha kufungwa kwa zahanati hiyo na kwamba ni kinyume cha sheria kwa watumishi wa afya kufunga zahanati na kuondoka wote kuelekea kwenye semina na kwamba atalifuatilia halmashauri kujua aliyetoa barua ya kwenda kwenye semina kwa watumishi na kufunga zahanati hiyo.

Aidha bwana Mbwiro amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watumishi hao mara tu itakapobainika wameondoka pasipo utaratibu nakuwataka radhi wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki wakati  taratibu za kuwatafuta wauguzi hao ili kuendelea kutoa huduma zikiendelea katika zahanati hiyo.

Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini bwana Deo Sanga amemuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kuhakikisha zahanati hiyo inafunguliwa mapema iwezekanavyo na kwamba watumishi

KESI YA DIWANI WA KATA YA RAMADHANI IMEENDELEA KUPIGWA KALENDA NJOMBE.

0 comments
Diwani wa Kata ya Ramadhani Bwana Alfred Luvanda  Ambaye Alishambuliwa na Kujeruhiwa na Katibu Mwenezi wa Kata Hiyo Bwana Erasto Ngole.

Kesi ya Kushambulia na Kumjeruhi Diwani wa Kata ya Raamadhani Alfred Luvanda Inayomkabili Katibu Mwenezi wa CCM kata ya Ramadhani Erasto Ngole Imeendelea Kuahirishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe kwa Kumkosa Shahidi wa Upande wa Mashtaka.

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama Hiyo Bwana Serapian Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa Shahidi wa Upande wa Mashtaka ambaye ni Dokta wa Hospitali ya Muhimbili ambaye alikuwa akimtibu Majeruhi Alfred Luvanda ameshindwa Kufika Mahakamani hapo.

Kwa mara Nyingine Tena Kesi Hiyo Imeahirishwa kwa Kumkosa Shahidi huyo ambapo awali Kesi hiyo Iliahirishwa Kutokana na
Shahidi Huyo kushindwa Kufika Mahakamani.

Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Ameahirisha Kesi hiyo Hadi Agosti 22 Mwaka Huu shahidi atakapofika Mahakamani Hapo.

ZAIDI YA ASKARI 3092 WAHITIMU MAFUNZO YAO MOSHI LEO.

0 comments

Tuesday, July 23, 2013

WANANCHI WAWACHONGEA WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA KWA MBUNGE.

0 comments


 Mbunge wa makete Dokta Binilith Mahenge Akipokea kero kwa wananchi wake.
 Wananchi wa Wilaya ya Makete waliowasemelea watendaji wa Vijiji na Kata kwa Mbunge wao Kwa kushindwa Kuwasomea Taarifa za Mapato na Matumizi kwa Muda Mwafaka.


Licha ya Serikali Kuwaagiza Watendaji wa Vijiji na Kata Kusoma Hesabu za Mapato na Matumizi Kila Baada ya Miezi Mitatu , Bado Agizo Hilo Linaonekana Kutotekelezwa na Baadhi ya Watendaji Hao Katika Mikoa Mbalimbali Ukiwemo Mkoa wa Njombe.

Hali Hiyo Imejitiokeza Wilayani Makete Baada ya Wananchi wa Kijiji cha  Ilovelo Kata ya Lupalilo Kulalamika Kutosomewa Taatifa ya Hesabu na Mapato na Matumizi Kwa Kipindi cha Takribani Miaka Mitatu Hadi Sasa.

Wakiongea Kwenye Mkutano wa Hadhara Mbele ya Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Makete Dk. Binilith Mahenge Wamesema Wamekuwa Wakichangia Fedha Kwa Ajili ya

Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo Kijijini Humo Ikiwemo Ujenzi wa Zahanati Lakini Hadi Hivi Sasa Hakuna Jitihada Zozote Zinazoonesha Kuanza Kwa Ujenzi Huo na Hakuna Taarifa Yeyote Inayoelezea Kutoanza Kwa Utekelezaji wa Miradi Hiyo.

Wamesema Kutokana na Uongozi wa Kijiji Hicho Kuwa Mbovu  Hawako Tayari Kuendelea Kuchangia Michango Kwa Ajili ya Miradi Yoyote Hadi Hapo Uongozi wa Kijiji Utakapobadilishwa .

Kufuatia Malalamiko ya Wananchi Hao Naibu Waziri Huyo wa Maji Dk. Mahenge Amemuagiza Diwani wa Kata Hiyo Pamoja na Katibu Tarafa wa Lupalilo Kwa Kushirikiana na Mkurugenzi Kuandaa Uchaguzi Katika Kijiji Kwa Ajili ya Kuwapata Viongozi Watakao Simamia Shughuli za Maendeleo Kwa Maslahi ya Wananchi.

SENGA NA PEMBE WATUA ARDHI YA NJOMBE.

0 comments

 Wachekeshaji Maarufu Nchini TANZANIA Senga na Pembe wafanya kufuru Njombe.
 Msanii Maarufu wa Nyimbo za Injili Tanzania anayetamba na Wimbo wa Chaguo lako Vanessah Sanga akifanya Maonesho kwa wakazi wa Njombe
 Maelfu ya Wakazi wa Njombe wakimbilia Uwanjani Sabasaba Kushuhudia Mbwembwe za
Senga na Pembe.






 Wakazi wa Njombe wakiwa Kuangalia Tamasha la Injili hasa wachekeshaji Maarufu Nchini SENGA na Pembe.
Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania Kulia ni Vanessah Sanga Maarufu kwa Ngoma ya Chaguo lako akiwa na Enock Jonas Anayetamba na Wimbo wa Zunguka zunguka wakifanya yao katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe Julai 21 Mwaka Huu.

Picha na Prosper Mfugale 

Tamasha la Injili Lililo andaliwa na MLOKOZI Intertainment Kutoka Mkoani Iringa Katika Uwanja wa Sabasaba Julai 21 Mwaka huu Limevunja Rekodi ya Kukonga Nyoyo za Mashabiki Hususani Pale walipo anza Mbwe mbwe akina SENGA NA PEMBE kATIKA Uwanja Huo Mjini Njombe.

Vichekesho vya Wachekeshaji Maarufu Kutoka Jijini Dar es Salaam WAKINA Pembe na Senga viliwaacha mashabiki Hoi wakiwa Stejini Katika Uwanja huo.

Pamoja na Tamasha Hilo Kuwaalika waimbaji wa Nyimbo za Injili Akiwemo Vanessah Sanga anayetamba na Wimbo wa Huyo ni chaguo Lako na Enock Jonas Anayetamba na Wimbo wa Zunguka zunguka ambao walialikwa Rasmi kwa ajili ya Tamasha Hilo Lakini Wachekeshaji hao walifanya kazi kubwa ya ziada ya Kujaza Mashabiki kwa Kiingilio cha Shilingi Elfu tatu kwa Elfu Mbili.

Saturday, July 20, 2013

NDUGU WATATU WAGONGANA NA MMOJA AFARIKI PAPO HAPO WILAYANI WANGING'OMBE NJOMBE LEO.

0 comments

>...Majeruhi wawili wakmibizwa Hospitali ya Ikonda Makete.
 
 Hiyo ndiyo Baiskeli iliyokuwa ikitumiwa na Marehemu kabla ya Mauti Kumkuta.
 Hii ndio Pikipiki iliyosababisha Ajali Mbaya Leo ya Mwendesha Baiskeli na Kusababisha Kifo Papo hapo.

 Hii ndio Barabara inayotumiwa kwa Kasi Kubwa baada ya Kulimwa na Hivyo Kusababisha Ajali za Mara kwa Mara Wilayani Wanging'ombe.

 Mwili wa Marehemu Linus Nziku mkazi wa Mdasi Wanging'ombe ukiwa Umefunikwa na Kuondolewa Katikati ya
Barabara alipogongwa.
 Mwendesha Baiskeli Marehemu Linus Nziku[45] aliyegongwa na Kufariki Papo hapo leo Asubuhi Katika Eneo la Nyaugao Mpakani Mwa Kijiji cha Makoga na Mdasi.


 Kona Iliyosababisha Ajali ya Mmoja Kufariki na Wengine Wawili Kujeruhiwa Vibaya na Kukimbizwa Katika Hospitali ya Ikonda Makete leo Asubuhi Huko Mdasi Wanging'ombe.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge akiwasili eneo la Tukio Hilo ambako alitakiwa Kufanya Mkutano na Wapiga Kura wake na Kisha Kulazimika kuahirisha Mkutano Huo.
 Hapa Mbunge Lwenge akitoa Pole katika Msiba Huo na rambi rambi ya Tshs.Laki Moja Barabarani Ulipotokea Msiba kabla ya Jeshi la Polisi Kuwasili Eneo Hilo.

Na Gabriel Kilamlya.

Mtu Mmoja Amefariki Dunia na Wengine Wawili Wamejeruhiwa Katika Ajali ya Pikipiki Iliotokea Leo Asubuhi Katika Kijiji Cha Mdasi Kata ya Makoga Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe.

Wakizungumza na Kituo Hiki Baadhi ya Mashuhuda wa Ajali Hiyo Akiwemo Diwani wa Kata ya Makoga Bw Abraham Chaula Amesema Ajali Hiyo Imetokea Leo Katika Barabara Kuu ya Njombe - Makete.

Amemtaja Mtu Aliefariki Kwenye Ajali Hiyo Kuwa ni Linus Nziku Mkazi wa Kijiji Cha Mdasi na Kusema Kuwa Majeruhi Wawili Wamekimbizwa Katika hospitali ya Ikonda Kwa Matibabu Zaidi.

Aidha Pamoja na Kuelezea Mazingira ya Tukio Hilo,Bw Chaula Amewashauri Watumiaji wa Vyombo Vya Usafiri Hasa Pikipiki Kuwa Makini Wanapokuwa Barabarani.

Jeshi la Polisi Limethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo.
................................................................................................

WALIOPISHA ENEO LA UJENZI WA MAKAO MAKUU WANGING`OMBE KUPEWA MASHAMBA MENGINE.

0 comments

 Huyu ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chalowe ambaye ameagizwa na Mbunge Kuwapa Mashamba wananchi waliopisha Eneo la Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging:ombe.


 Naibu waziri wa Ujenzi akiagiza SERIKALI YA kijiji cha Chalowe Kuwapa Mashamba Wakulima waliopisha Eneo la Ujenzi wa MAKAO MAKUU ya Wilaya ya Wanging`ombe.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge Ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi ameuagiza Uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Chalowe Kata ya Igwachanya kuwapa Mashamba ya Kulima wananchi waliopisha Eneo la Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Kitongoji cha Wangama.

Agizo Hilo amelitoa jana wakati wa Ziara yake katika Kitongoji Hicho ikiwa ni Muendelezo wa Ziara Jimboni kwake na Kwamba kitendo cha Wananchi Kukubali kutoa Eneo Hilo kwa ajili ya Ujenzi Huo ni Jambo la Busara Hivyo kama serikali ya Kijiji inapaswa kuwaonesha eneo Jingine la Kulima haraka Iwezekanavyo.

Awali wananchi hao wamesema walishatoa Ombi la Kupatiwa eneo Jingine kwenye Ofisi ya Kijiji hadi Kwa Mkuu wa Wilaya lakini Jambo Hilo halikutekelezwa hali iliyopelekea Mbunge Huyo kuagiza Kuwashughulikia

wananchi Hao ili kuanza Ujenzi Haraka.

Jafary Gidion ni Mwananchi wa Kitongoji cha Wangama ambaye  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa  Wakulima Hao Katika eneo yatakakojengwa makao makuu ya Wilaya Hiyo,hapa akasimama na Kupaza sauti yake kwa Mbunge kwa Niaba ya Wakulima Juu ya Eneo Hilo.

Mbunge Lwenge alipofika katika Kijiji cha Igwachanya ambako ndiko Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe akakutana na Maswali Mbalimbali ya Wananchi Likiwemo la Kutaka Kupewa Ufafanuzi Juu ya Kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa Bungeni iliyoeleza Juu ya Kuwapiga Raia watakao leta usumbufu kwa Jeshi la Polisi.



 Mbunge Lwenge akizungumza na Wananchi wa Kitongoji cha Wangama Leo
 Hawa ni wananchi wa Kitongoji cha Wangama Kijiji cha Chalowe waliohoji juu ya Wao kutoa Eneo la Ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Wilaya ya Wanging`ombe Bila Kupewa Mashamba Mengine.

Hapa ni Igwachanya karibu na Ofisi za Kata ya Hiyo.

Wananchi wa Kijiji cha Igwachanya wakisikiliza Majibu ya Mbunge wao Baada ya Kumuuliza Maswali kadha wa kadha.

Na Gabriel Kilamlya.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge Ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi ameuagiza Uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Chalowe Kata ya Igwachanya kuwapa Mashamba ya Kulima wananchi waliopisha Eneo la Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Kitongoji cha Wangama.

Agizo Hilo amelitoa jana wakati wa Ziara yake katika Kitongoji Hicho ikiwa ni Muendelezo wa Ziara Jimboni kwake na Kwamba kitendo cha Wananchi Kukubali kutoa Eneo Hilo kwa ajili ya Ujenzi Huo ni Jambo la Busara Hivyo kama serikali ya Kijiji inapaswa kuwaonesha eneo Jingine la Kulima haraka Iwezekanavyo.

Awali wananchi hao wamesema walishatoa Ombi la Kupatiwa eneo Jingine kwenye Ofisi ya Kijiji hadi Kwa Mkuu wa Wilaya lakini Jambo Hilo halikutekelezwa hali iliyopelekea Mbunge Huyo kuagiza Kuwashughulikia wananchi Hao ili kuanza Ujenzi Haraka.

Jafary Gidion ni Mwananchi wa Kitongoji cha Wangama ambaye  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa  Wakulima Hao Katika eneo yatakakojengwa makao makuu ya Wilaya Hiyo,hapa akasimama na Kupaza sauti yake kwa Mbunge kwa Niaba ya Wakulima Juu ya Eneo Hilo.

Mbunge Lwenge alipofika katika Kijiji cha Igwachanya ambako ndiko Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe akakutana na Maswali Mbalimbali ya Wananchi Likiwemo la Kutaka Kupewa Ufafanuzi Juu ya Kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa Bungeni iliyoeleza Juu ya Kuwapiga Raia watakao leta usumbufu kwa Jeshi la Polisi.

Kufuatia Swali hilo Lwenge akasimama na kutolea Majibu ambapo hata yeye akarudia Kauli hiyo na Kusema"hata mimi na Sema Pigeni"


Kauli hiyo ameitoa kutokana na Kwamba Waziri Mkuu alieleza Hivyo kwa Kuwa Tayari Baadhi ya Wananchi Mtwara walishaingia Vitani wakiwa na Silaha kwa Kuchoma Madaraja,KUCHOMA Nyumba za Viongozi na Hivyo Bila Mapigano kwa silaha isingewezekana.

Ziara Hiyo Kesho inaendelea Katika vijiji Vinne vya Kata ya Ulembwe na Makoga kabla ya Kuhitimisha Julai 19 Mwaka Huu.

MADIWANI WALIA NA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI

0 comments
Mkuu wa wilaya ya makete bi Josephine Matiro

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya makete wamelalamikia utendaji mbovu wa watendaji  wa vijiji na kata ambapo zaidi ya watendaji ishirini waliopo  katika kata ishirini na mbili  wamedaiwa kujihusisha na unywaji pombe hali inayopelekea kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Wakitaja majina ya watendaji  na hali  utendaji wao wa kazi  madiwani  katika kikao cha robo ya nne  ya mwaka 2012/2013   wamasema kuwa pamoja na upungufu  wa watumishi   hao   lakini waliopo wana matatizo mbalimbali  yakiwemo ulevi na utoro wa kuto kukaa katika vituo vyao vya kazi hadi kusababisha kushindwa kukusanya mapato na kuiingizia hasara  halmashauri hiyo.

Pia katika baraza hilo wakiendelea kutoa malalamiko hayo wamesema kuwa katika kata zao kuna upungufu wa watumishi hao ishirini na moja  na watumishi wengine waliopungufu ni maafisa mifugo na  kilimo.


kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw Idd Nganya amekiri kuwepo kwa upungufu huo  na kusema kuwa  uuondoshwaji wa watumishi hao bila taarifa katika sehemu zao za kazi bila taarifa kwa baadhi ya viongozi  wakiwemo madiwani katika kata zao

Pia mkurugenzi mtendaji huyo  amewataka madiwani hao  kuacha tabia ya kuwakataa baadhi ya viongozi  wakiwemo wanaohamishwa kutokana na matatizo wanayokutwa nayo katika  vituo vyao vya awali.

Aidha Baraza hilo lililoishia hapo jana   limepitisha waraka wa kuwafukuza kazi watumishi nane wa sekta mbalimbali wakiongozwa na wauuguzi  na maafisa ugani kutokana na tatizo la utoro wa muda mrefu

Baraza hilo pia limemchagua Aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Jison John mbalizi kuendelea kushikiria wadhifa huo sambamba na uchaguzi wa kamati mbili na wenyeviti wao.